LATEST NEWS FOR MORE INFO

RIHANNA NA CHRIS BROWN KTK PICHA YAO MPYA


Wiki moja baada ya mwimbaji Rihanna kupost kwenye page yake ya mtandao wa Instagram picha ya Chris Brown akiwa kitandani bila shati, time hii Rihanna amezidi kuvipa vyombo vya habari cha kuongea baada ya kupost picha nyingine.Picha yenyewe ni hiyo hapo kushoto ambapo sasa inazidi kujulikana kabisa kwamba Rihanna na Chris Brown ambao ni wapenzi wa zamani wamerudiana japo hawajawahi kutamka.
Kwa mujibu wa Necole, baada ya kuiweka hii picha RiRi aliandika “I don’t wanna leave! Killed it tonight baby”Kwenye moja ya interview zake mwaka huu, Rihanna alisema bado moyo wake unamkubali sana Chris Brown na ni ngumu kumsahau maishani.Picha hizi za Instagram zimezagaa siku kadhaa tu baada ya Chris Brown kutangaza kwamba ameachana na mpenzi wake ili kurejesha amani manake hakua anapenda akiona urafiki wa Chris na Rihanna unaendelea.

UJUMBE WA MWISHO WA SHARO MILLIONEA BAADA YA KUCHAT NA LINEX

Huu ni ujumbe kutoka kwa marehemu baada ya ku chart na msanii wa Bongo Fleva hapa Tzee almaarufu kama Linex Sunday.

MSANII SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA


Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
DENI LA MILIONI MOJA LAMPA WAKATI MGUMU MSANII HEMED AKA PHD

UKWELI wa mambo juu ya msanii anayependa kulipuka pamba *Hemed Suleiman ’Hemedi’* almaarufu kama PHD au Alejandro, umevuja kwani inadaiwa kuwa nguo zote anazoonekana anavaa huwa anachukua kwa mkopo na hulipa baada ya muda fulani lakini sasa kiasi cha fedha anachodaiwa ni kikubwa na hana uwezo wa kulipa kwa sasa kwani ni zaidi milioni 1. Duka moja la nguo maarufu sana lilipo maeneo ya Kinondoni, ndilo lililotoa ishu hiyo baada kuona jamaa huyo anazingua kulipa na walikuwa wakimpa kila nguo anayohitaji kwani walimuamini kwa kuwa nguo nyingi alikuwa akinunua hapo kwao. Muuzaji wa pamba hizo katika duka hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe na duka pia, alisema kuwa awali jamaa alikuwa akilipa kama kawaida lakini ilifika kipindi alikuwa anachukuwa kila baada ya wiki na hadi hivi sasa anadaiwa si chini ya milioni 1. /“Hemedi tunamuamini lakini sasa hali hii inafikia kuwa vita kwa sababu kiasi cha fedha tunachomdai ni kikubwa kwa sababu watu wanafanya kazi wanahitaji kulipwa mshahara, tunafikilia kuchukua maamuzi ili aweze kutulipa kwa haraka. Jamaa sikuhizi haji hapa na wala sijamuona kupita sasa sijui anakimbia madeni au vipi,” /aliongeza Hata hivyo*Hemedi *alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo kama ina ukweli wowote hakuweza kupatikana na taratibu zinaendelea za kumtafuta ili aweke wazi juu ya habari hizo.

 
  MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, amepatwa na kile kinachoonekana ni balaa nambari moja tangu apate umaarufu. Gari la Diamond aina ya Toyota Land Cruiser Prado TX baada ya kugongana na Toyota Rav 4. Jumamosi iliyopita, Diamond akiwa anaendesha gari lake la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser Prado TX, aligongana na Toyota Rav4, lililokuwa linaendeshwa na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijapatikana. Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, Diamond aligongana na mwanamke huyo kwenye Barabara ya Kimweri, Msasani, Dar es Salaam,saa 3 usiku. Kenyela… .
HUYU NDIYE MISS TZ 2012

LORD EYEZ AIBU MAHAKAMANI



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka Kundi la Nako 2 Nako Soldiers, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, Ijumaa iliyopita alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka sita ya wizi wa vitu mbalimbali yanayomkabili.

 
Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ akipelekwa kwa 'Pilato'.


H-BABA ADAI KUWA DAIMOND AMECHUKUA IDEA YA NYIMBO YA NATAKA KULEWA KUTOKA KWAKE



H.Baba akionesha cd na flash zenye demo ya wimbo wake (Nataka Kulewa)
H.baba ametoa exclusively kipande cha wimbo wake uitwao ‘Nataka Kulewa’ kupitia BONGO 5 ambao amemshirikisha Q-Chief. Msanii huyo anamshutumu Diamond kuiba wazo na jina la wimbo wake huo katika wimbo wake mpya wenye jina kama hilo.
Tumefanya naye mahojiano ambayo utayaangalia muda mfupi ujao kupitia hapa hapa lakini kwa sasa usikilize wimbo huo hapa ambao bado ni demo.

                      SIKILIZA HAPA KUPITIA BONGO 5 JUST CLICK
 
Support : Copyright © 2013. MKATOLIKI ASILIA - All Rights Reserved
Template Created by Titus kapoma Published by KAPOMACLAN CO
Proudly powered by Blogger