DENI LA MILIONI MOJA LAMPA WAKATI MGUMU MSANII HEMED AKA PHD
UKWELI wa mambo juu ya msanii anayependa kulipuka pamba *Hemed
Suleiman ’Hemedi’* almaarufu kama PHD au Alejandro, umevuja kwani
inadaiwa kuwa nguo zote anazoonekana anavaa huwa anachukua kwa mkopo na
hulipa baada ya muda fulani lakini sasa kiasi cha fedha anachodaiwa
ni kikubwa na hana uwezo wa kulipa kwa sasa kwani ni zaidi milioni 1.
Duka moja la nguo maarufu sana lilipo maeneo ya Kinondoni, ndilo
lililotoa ishu hiyo baada kuona jamaa huyo anazingua kulipa na walikuwa
wakimpa kila nguo anayohitaji kwani walimuamini kwa kuwa nguo nyingi
alikuwa akinunua hapo kwao.
Muuzaji wa pamba hizo katika duka hilo ambaye hakupenda jina lake
litajwe na duka pia, alisema kuwa awali jamaa alikuwa akilipa kama
kawaida lakini ilifika kipindi alikuwa anachukuwa kila baada ya wiki na
hadi hivi sasa anadaiwa si chini ya milioni 1.
/“Hemedi tunamuamini lakini sasa hali hii inafikia kuwa vita kwa sababu
kiasi cha fedha tunachomdai ni kikubwa kwa sababu watu wanafanya kazi
wanahitaji kulipwa mshahara, tunafikilia kuchukua maamuzi ili aweze
kutulipa kwa haraka. Jamaa sikuhizi haji hapa na wala sijamuona kupita
sasa sijui anakimbia madeni au vipi,” /aliongeza
Hata hivyo*Hemedi *alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo kama ina ukweli
wowote hakuweza kupatikana na taratibu zinaendelea za kumtafuta ili
aweke wazi juu ya habari hizo.
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na
Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA
-
Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).
Kauli ya hiyo ya Bunge im...
11 years ago




0 comments:
Post a Comment